Baadhi ya Pikipiki kati ya 35 na magari 10 yatayosambazwa katika mikoa mbali mbali, baada ya kukabidhiwa leo jijini Dar es salaam, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kwa uongozi wa Mikoa kwaajili ya kwenda kusimamia, na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mikoa mbali mbali waliokabidhiwa piki piki 35 na magari 10 leo jijini Dar es salaam.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu moja ya
piki piki kati ya 35 zitakazosambazwa katika mikoa mbalimbali kwenye
hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10
na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu
wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia
kwa wakati.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata ufunguo wa
moja ya gari kati ya 10,yatakayosambazwa katika mikoa 10 ,hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi
magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha
Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma
zinawafikia kwa wakati.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye moja ya magari hayo kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
Na WAMJW - DSM
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi magari 10 na
pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali nchini huku akisisitiza Serikali ya
Awamu ya Tano imejikita kuboresha sekta ya huduma ya afya kwa
Watanzania.
Magari na
pikipiki amekabidhi leo Januari 14, 2019, Mwalimu amesema tukio hilo la
kukabidhi rasmi Magari 10 na Pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa kwa ajili
ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za
Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo ni muhimu .
"Kama
mnavyofahamu bado nchi yetu inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Kifua
Kikuu (TB) na Ukoma. TB ni hatari kwani inasababisha vifo, na Ukoma
husababisha vifo na ulemavu wa kudumu. TB pia inaongoza kusababisha vifo
vingi miongoni mwa wananchi wenye VVU," amefafanua Waziri Mwalimu.
Ameongeza
kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB wapatao
154,000 ambao kati yao ni 44% (69,818) tu ndio waliogunduliwa.
Changamoto kubwa ni jinsi ya kufikishia wananchi wote huduma za kufanya
uchunguzi na upimaji pamoja na kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu
magonjwa hayo.
Ameongeza
Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa inafanya jitihada kubwa kuhakikisha
wananchi wanapata huduma hizo ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa ugonjwa
wa TB na kwamba mojawapo ya juhudi hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine
za kupima vinasaba vya Kifua Kikuu kitaalamu Gene-Xpert.
Ambapo
zimeongezeka kutoka 64 mwaka 2015 hadi 210 Disemba 2018 na kufanya 85%
(158/186) ya Halmashauri zote nchini kuwa na mashine hizi zinazoweza
kupima TB kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.
"Mashine
hizo hutoa majibu ndani ya saa 2 tofauti na kipimo cha Hadubini ambazho
huto majibu baada ya saa 48. Lengo ni hadi kufikia mwisho wa mwaka huu
wilaya zote ziwe na mashine hizi. Kipimo hiki cha Gene-Xpert hutolewa
bure," amesema.
Waziri
Mwalimu amesema Serikali hiyo imepeleka huduma ya kifua kikuu sugu
karibu kwa wananchi, huduma ambayo wakati Serikali ya awamu ya tano
inaingia madarakani ilikuwa inapatikana katika hospitali moja tu ya
Kibong’oto lakini kwa sasa inapatikana katika vituo 81 katika mikoa 23.
"Ni
katika kuongeza juhudi hizi, Serikali kupitia Wizara imenunua magari 10
na pikipiki 35 tunazozikabidhi leo kwa lengo la kuhakikisha Waratibu
hawa wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma
zinawafikia kwa wakati.
"
Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki
35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538. Jumla ni milioni 778. Mikoa
inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi,
Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa.
"Pikipiki
35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu,
Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu,
Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje,
Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo,
Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na
Gairo ," amefafanua.
Pia
amesema magari hayo na Pikipiki zinazokabidhiwa kwa uongozi wa mikoa
vitasaidia katika usimamizi wa shughuli za Mpango, kuhakiksha wagonjwa
wa TB na Ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.
Amesema
vyombo hivyo vitatumika kwa shughuli zinginezo za mikoa na wilaya
zinazolenga kumfikishia huduma bora za afya mwananchi. Ametoa rai yake
kwa uongozi wa Mikoa inayopatiwa vyombo hivyo vya usafirishaji vitumike
kwa shughuli iliyokusudiwa kuimarisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma.
Amesisitiza
vyombo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo na
wanaamini kwamba Mikoa hiyo itaongeza kwa kasi ugunduzi wa wagonjwa wa
Kifua Kikuu na kutokomeza ugonjwa wa Ukoma katika mikoa yenu.
Ameongeza
lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 tunawaibua na kuwapatia
matibabu asilimia 70 ya watu wanaougua TB kutoka asilimia 48 ya hivi
sasa.
Waziri Mwalimu
amesema kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma ni malengo ya Serikali kutokomeza
ugonjwa huo katika Wilaya 20 zilizobakia ambazo ni Liwale, Mkinga,
Nkasi, Lindi DC, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga Manispaa, Kilombero,
Mafya, Pangani, Mvomero, Masasi, Chato, Mpanda TC, Nachingwea, Rufiji,
Korogwe, Ulanga, Morogoro DC na Kilwa DC.
Ametumia
nafasi hiyo shukurani kwa Mfuko wa Dunia (GF – ATM) kwani, fedha hizo
ni sehemu ya mfuko huu wa mzunguko wa 2018 – 2020.
Baadhi
ya piki piki kati ya 35 na Magari 10 yatakayosambazwa katika mikoa
mbalimbali, zilizokabidhiwa leo jijini Dar na Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa uongozi wa mikoa kwa
ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa
huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo.
Mikoa
10 inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi,
Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa na Pikipiki 35 zinatolewa kwa
Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa,
Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali,
Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana,
Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara,
Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo.
Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538
0 on: "WAZIRI UMMY AKABIDHI MAGARI 10,PIKIPIKI 35 KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA AFYA"