Na WAMJW - NYASA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wiki mbili na kuwaagiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwachukulia hatua Kali wabadhilifu wote waliohusika katika kuhujumu ujenzi wa kituo cha Afya Mkili kilichopo katika Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya, uboreshaji wa miundombinu na uhamasishaji kwa wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo yao wenyewe mkoani Ruvuma.
Dkt. Ndugulile alisema hatua Kali za haraka zitachukuliwa kwa yeyote aliyehusika kwa namna yoyote ile katika kukihujumu kituo hicho na kusisitiza kwamba hatobaki salama," kituo ambacho kilikuwa moja kati ya vituo vya Afya vilivyopewa Fedha za ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa baadhi ya majengo ya Afya".Alisisitiza Dkt.Ndugulile.
"Ofisi ya Rais TAMISEMI wafuatilie hili na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa ili Wizara ya Afya ipate taarifa hiyo ya nini kinachojiri, walichokibaini ni nini, hatua ambazo wanachukua na muendelezo wa ujenzi huu" alisema Dkt. Faustine ndugulile.
Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali hii haitomvumilia mtu yeyote anayecheza na Fedha za dawa, hivyo kumwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Majura Magafu kupitia vyanzo vyote vya mapato ambavyo Serikali inapata kupitia CHF, BIMA YA AFYA, na vyanzo vyote vya papo kwa papo kisha kuangalia matumizi yake ya Fedha.
"Matumizi mabaya ya Fedha za dawa, sasa hilo nalo linahitaji lichunguzwe, Rmo naomba hili lifanyiwe kazi haraka, mkapitie vyanzo vyote vya mapato ambavyo tunapata kupitia CHF, BIMA YA AFYA, na vyanzo vyote vya papo kwa papo na tuangalie matumizi ya Fedha yakoje" alisema Skt Ndugulile.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, huku akitoa maelekezo ujenzi Wa Hospitali hiyo uanze mara moja, huku akisisitiza kuwa utaratibu utaotumika ni wa Forced Account (mafundi wakawaida na wananchi kushiriki katika ujenzi ) jambo litakalosaidia kuokoa Fedha nyingi, zitazosaidia kuboresha sekta ya Afya.
"Tumeleta milioni 400, na tumeleta Bilioni 1.5, hizi fedha zipo, mkurugenzi wa halmashauri yuko hapa, na natoa maelekezo ndani ya muda mfupi ujenzi uanze, utaratibu ni kutumia mafundi, nyie wenyewe wa Nyasa mtajenga Hospitali yenu." Alisema Dkt. Ndugulile
Naye Mjumbe wa kamati ya ujenzi katika kituo cha Afya Mkili Bw.John Ngamanyika amemshutuma mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa Bw.Dkt Oscar Mbyuzi kwa upigaji wa pesa hizo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kumalizika kwa kituo hicho ambacho kilipewa na Serikali jumla ya shilingi Milioni 400 kwa ajili ya kuboresha kituo hicho.
"Mheshimiwa Naibu Waziri fedha zilizotengwa katika kituo cha Afya Mkili shilingi milioni 400, mimi nakuhakikishia zingetosha kabisa kumalizia majengo haya, , hapa kilichotawala ni wizi, na anayeongoza ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya" alisema Bw. John Ngamanyika.
Bw. John Ngamanyika aliendelea kusema kuwa Mwenyekiti wa bodi ya kituo cha Afya pamoja na Katibu wake wameshikiliwa na polisi kwa wizi wa sementi na kwa sasa wanasubiri jarada lao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa uhujumu huo.
Mwisho.
0 on: "WALIOHUJUMU UJENZI WA KITUO CHA AFYA MKILI WACHUKULIWE HATUA-DKT.NDUGULILE"