Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Baadhi ya wakuu wa idara kutoka mkoa na wilaya wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa(hayupo pichani)ambapo wametakiwa kuhamasisha utekelezaji wa kuwaibua wagonjwa wa ukoma kutoka kila kaya ili kufanikisha malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma ifikapo mwaka 2020
Picha ya pamoja ya viongozi wa Mkoa, Wilaya,Wizara ya Afya na GLRA mara baada ya ufunguzi
Na.WAMJW,Morogoro
Wananchi
wa Mkoa wa Morogoro na halmashauri zake wametakiwa kutowaficha wagonjwa wenye
ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa hadi ifikapo mwaka 2020.
Hayo
yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari wakati wa
ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uongozi
wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya mvomero kuhusu maadhimisho ya miaka
sitini (60) ya Ushirikiano kati ya serikali na Shirika la German Leprosy and Tb
Relief nchini Tanzania(GLRA) pamoja na siku ya ukoma Duniani itakayofanyika
Kitaifa wilayani Mvomero mwishoni mwa mwezi huu
“Serikali
inawajali sana wananchi wake hivyo
wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya
kutolea huduma za afya nchini” Alisema Tandari
Aidha,
alisema kuwa mkoa wake utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza ugonjwa wa ukoma mkoani hapa kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu hao kupona
na kurudi kwenye kazi zao za kila siku watu wagonjwa hao wakishapatiwa dawa
wanapona kabisa.
Kwa
upande wa ongezeko la wagonjwa wilayani
Mvomero Katibu Tawala huyo alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa
wagonjwa hao wilayani hapo ni muingiliano hususan kwenye mashamba hivyo inakua
rahisi maambukizi kuwa juu”tutafanya jitihada ili kuweza kufikia viwango vya
Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kutokomeza ugonjwa huu ambapo malengo ni mgonjwa mmoja kati ya watu elfu kumi.
Naye
Mratibu wa Taifa wa ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Deus Kamara alisema kuwa zipo halmashauri 20
ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ukoma nchini hivyo wizara kupitia
mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, Mikoa inatakiwa kutengeneza
mkakati wa kuwasaka,kuwafikia, kuwaibua
na kuwaweka katika matibabu stahili pamoja na kuzifikia kaya zote zenye
wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua kuwapatia tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri
zote ifikapo mwaka 2020.
Wakati
huo huo Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA Buchard Rwamtoga alisema kuwa
shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka sitini(60) hapa nchini katika
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa ukoma
Tanzania ikiwemo ya kuwajengea makazi bora familia 120 kutoka familia 739 ya
watu waliougua ukoma hapa nchini
“Dhamira
yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali,shirika
linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa mpango wa taifa wa
kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na Ukoma kupunguza madhara yatokanayo na
magonjwa haya”alisisitiza Rwamtoga.
Alitaja
mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 Mwakilishi Mkazi huyo alisema shirika lake
wameweza kutoa viatu maalum kwa walioathirika na ukoma pea 94,500 kwa watu 47,
250, miguu bandia magongo na baiskeli kwa watu 2, 655, magari 270 kwa Tanzania
bara na Zanzibar,kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na
kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50 vyenye wanachama 677 kwa familia
za watu wenye kuishi na ugonjwa wa Ukoma nchini.
Kauli
mbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu ni “Tutokomeze ubaguzi
,Unyanyapaa na chuki dhidi ya waathirika wa Ukoma” na kitaifa yatafanyika
kwenye kitongoji cha Chazi kijiji cha kigugu Wilayani Mvomero tarhe 27 mwezi
huu.
-Mwisho-
0 on: "MOROGORO WATAKIWA WASIFICHE WAGONJWA WA UKOMA MAJUMBANI"