Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 6 Januari 2019

WAZIRI MKUU AMWAGIZA NAIBU WAZIRI WA AFYA KUFUATILIA UHUJUMU WA JENGO LA MAMA NA MTOTO.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati aliponya ziara ya uzinduzi wa Mashine ya X- Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma wakati aliponya ziara ya uzinduzi wa Mashine ya X- Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Pembeni yake ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali mgonjwa  aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua mashine mpya ya X-ray aliyoizindua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile, anaefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mdeme.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine ya X-ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile, wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe. Christina Mdeme, wapili kushoto ni Mbunge wa Songea Mhe. Damas Ndumbalo.


Na WAMJW - SONGEA

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  amemwagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kufuatilia uhujumu wa Fedha za ukarabati wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Ameyasema hayo jana wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuzindua X-Ray Mashine za kisasa katika Mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Milioni 500 inajenga kituo kizima cha Afya, ambacho kina chumba cha uoasuaji'thieta', wodi ya mama na mtoto, jengo la wagonjwa wa nje,  nyumba ya Mtumishi, mochwari na kichomea taka, hapa jengo moja linalofanana na thieta ni Milioni 129 kule ni Milioni 70, hii haikubaliki hata kidogo.

'Waziri utabaki hapa, utafuatilia hiyo, tujue nani aliyeweka zabuni hiyo, tushughulike nae, hatuwezi kuruhusu hali hii, na tukiendelea hivi tutaharibu kila kitu, lazima tuelezane ukweli, Serikali tumetaka kuboresha sekta ya Afya, tumetafuta mfumo mzuri, tunafedha, na tunaendelea kujenga, sasa kuna watu wanaingia huko wanataka kutuharibia" alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Mbali na hayo Mhe. Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali huzipatia Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kiasi kisichopungua Milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa Dawa kila mwezi, huku akiwatoa hofu Wananchi kuwa Dawa zipo na zimefikia Asilimia 92.

"Kila mwezi, halmashauri chini kabisa inayopata Fedha za dawa pekee, sio chini ya Milioni 25 kwa mwezi, kwa miezi mitatu ni shilingi Milioni 75, na Fedha hizi zinakuja na wananunua dawa moja kwa moja, dawa  zipo, na zimefikia Asilimia 92℅ na kuendelea" alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Mhe. Kassim Majaliwa aliendelea kuwahasa Wasimamizi wote waliopo katika vituo vya Afya, kuhakikisha kuwa Dawa za matibabu zinatumiwa vizuri, na zitumike kwa kuwapa Wananchi waliopata maradhi 

"Leo nimeingia kwenye wodi ya watoto wadogo, nimekutana na mtu mmoja aliyekuwa na malalamiko ya dawa, inawezekana mtu, mmoja anataka kuwachafua wengi, kwasababu wote mnajua hapa dawa zipo na mgonjwa atapata Dawa' alisema Mhe. Kassim Majaliwa.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alitoa rai kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma juu ya masuala ya lishe, huku akiwahasa viongozi wa Mkoa kuhamasisha Wananchi ili wafahamu juu ya umuhimu wa Lishe bora.

" Nisisitize masuala ya Lishe, iwe ni ajenda ya kudumu, Mkoa wa Ruvuma unazalisha chakula kwa wingi, lakini sasa ndio unaongoza kwa matatizo ya utapiamlo, maana yake ni kwamba, hatujui namna ya kula" alisema Dkt. Ndugulile

Mwisho
0 on: "WAZIRI MKUU AMWAGIZA NAIBU WAZIRI WA AFYA KUFUATILIA UHUJUMU WA JENGO LA MAMA NA MTOTO."