Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Josephat Maganga (kulia)
wakitoka kukagua jengo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyekuja kupata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita. Katikati ni mama wa mtoto huyo Bi. Jenista Benedicto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiangalia ramani ya majengo za majengo ya Hospitali ya rufaa ya Geita
wakati alipotembelea ujenzi huo. Pembeni ni msimamizi wa ujenzi huo
Injinia Grace Elias.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiangalia mashine mpya ya X-ray ya kidigitali iliyifungwa katika
Hospitali ya wilaya ya Chato wakati alipoitembelea hospitali hiyo kuona
hali ya utoaji huduma za afya.
HOSPITALI YA MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA
Na WAMJW-GEITA
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameuagiza uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Geita kuhakikisha wanafungua
duka la dawa ili kutoa huduma karibu na wananchi pia kuongeza mapato ya
Hospitali.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo mapema leo
wakati alipoitembelea hospitali hiyo ili kuona hali ya miundombinu
pamoja na utoaji wa huduma za afya.
“Tumeshaagiza
Hospitali zote nchi nzima kuwa na maduka ya dawa ya Hospitali, kwanini
hapa hamjafungua duka lenu? Alihoji Waziri Ummy na kuongeza “sasa nawapa
miezi miwili uongozi wa Hospitali kuhakikisha mnafungua duka la dawa la
Hospitali ili liweze kuwasaidia kupandisha mapato lakini pia kusogeza
huduma karibu na wananchi. Alisema Waziri huyo.
Pamoja
na hayo Waziri Ummy ameonekana kuridhishwa na hali ya upatikanaji wa
dawa wa zaidi ya asilimia 90 na uboreshwaji wa huduma za afya
zinazotolewa katika Hospitali hiyo.
Kabla ya hapo
Waziri Ummy alitembelea ujenzi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita
ambapo alishuhudia ujenzi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 54 lakini
amemtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi huo ambaye ni wakala wa ujenzi
(TBA) kufanya kazi usiku na mchana ili Hospitali hiyo ianze kufanya kazi
ifikapo Mwezi Julai 2019.
Waziri Ummy amekamilisha
ziara yake ya mkoa wa Geita kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Chato
ili kujiridhisha na hali ya utoaji wa huduma za afya na miundombinu
pamoja na kuhakikisha kama vifaa na vifaa tiba vinapatikana Hospitalini
hapo.
Waziri Ummy ameridhishwa na utolewaji wa
huduma za afya lakini ameitaka Hospitali hiyo kuwa na chumba maalum
chenye vifaa maalum vya uangalizi wa watoto wachanga mahututi na wale
waliozaliwa kabla ya siku (watoto njiti) lengo likiwa ni kupunguza vifo
vya watoto wachanga nchini.
Aidha, waziri huyo
ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuanzisha kitengo cha huduma za
wagonjwa wa dharura na wale waliopata ajali ikiwa ni agizo la serikali
kwa hospitali zote za wilaya na mikoa nchi nzima.
Huo
ni muendelezo wa ziara za Waziri Ummy katika mikoa ya kanda ya ziwa
kutembelea Hospitali mbalimbali kuangalia hali ya miundombinu na utoaji
wa huduma za afya.
0 on: " HOSPITALI YA MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA"