Jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini KCMC.
Mwaka
2018 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa ilikuwa 42,411,276 katika vituo vya
kutolea huduma za tiba nchini ikilinganishwa na 54,478,926 kwa mwaka 2017 Kati
ya hao wagonjwa wa wa nje (OPD) ilikuwa 41,052,012 na wagonjwa wa kulazwa (IPD)
ilikuwa 1,359,264.
1.
Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na
Zahanati katika ngazi ya msingi.
Ø Katika mwaka 2018 jumla ya wagonjwa wa nje (OPD) ilikuwa
36,376,967 walipatiwa huduma katika hospitali za Halmashauri, hospitali
nyingine, vituo vya afya na zahanati ikiwa ni 18,194,619 hudhurio la kwanza na
18,182,348 mahudhurio ya marudio. Mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wa nje (OPD)
ilikuwa 47,650,158 ambapo 30,174,341 hudhurio la kwanza na 15,809,971
mahudhurio ya marudio.
Wakati
huo huo wagonjwa wa Kulazwa mwaka 2018 walikuwa 404,659 ikilinganishwa na
wagonjwa 523,587 mwaka 2017
2.
Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa mwaka 2018
Ø Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2018 Hospitali za
Rufaa za Mikoa zilihudumia jumla ya wagonjwa 3,526,503 ambapo wagonjwa wa nje
walikuwa 3,054,318 na wagonjwa wa ndani walikuwa 472,185 ikilinganishwa na
wagonjwa 4,781,999 waliohudumiwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2017.
3.
Mahudhurio ya wagonjwa katika Hospitali ya Taifa, Hospitali Maalum na Hospitali
za Rufaa za Kanda
Ø Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2018, Hospitali
hizi zilihudumia jumla ya wagonjwa
2,103,147 ambapo wagonjwa wa kulazwa walikuwa 482,420 na wagonjwa wa nje
walikuwa 1,620,727. Ikilinganishwa na idadi ya wangonjwa 2,046,769 kwa kipindi
cha Januari hadi Desemba 2017. Ambapo idadi ya wagonjwa wa kulazwa ilikuwa
711,766 na wagonjwa wa nje 1,335,003.
Imetolewa
na;
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
0 on: "HALI YA HUDUMA ZA TIBA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018"