Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bw.Adam Fimbo akizungumza na maofisa habari wa
wizara na taasisi(hawako pichani) jinsi mamlaka hiyo ilivyokuwa na
mifumo bora ya udhibiti na kuifanya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika
katika kampeni ya "Tumeboresha sekta ya Afya"
Kaimu Meneja wa kitengo cha Maabara Micro Biology ya TFDA Catherine Luanda akiwaeleza jambo Maafisa Habari wa Wizara na Taasisi zake namna ya utendaji kazi katika maabara hiyo
Na WAMJW - Dar es Salaam
Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu
imeweza kufanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na
usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa
kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015.
Hii
ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu ya utekelezaji wa kazi chini
ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea
katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa,
vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Adam Fimbo amebainisha hayo wakati akitoa
ripoti ya miaka mitatu ya Mamlaka hiyo wakati wa ziara maalum ya
Maafisa Mawasiliano na habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika
kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza
mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
"Kutokana
na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa
dawa, mnamo Mwezi Desemba 2018, TFDA imetambulika kufikia ngazi ya tatu
(Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa
udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vipodozi, ambapo hatua hii imeifanya
Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hii
Fimbo
ameeleza kuwa, TFDA katika mikakati yake hiyo imeweka mifumo na
taratibu za ndani za utoaji huduma na utendaji bora ili kukidhi
mahitaji na matarajio ya wateja kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya
ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida na ISO 17025:2005 kwa huduma za
maabara.
Aidha,
ameongeza kuwa huduma za TFDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya
Mkataba wa Huduma Wateja kama ulivyorejewa mwaka 2016.
"Mfumo
wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi
ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi
vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, katika kipindi cha
2015/16 hadi 2017/18.
Pia
tumesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa
zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Hii
imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa
wafanyabiashara na kukua kwa biashara." Ameeleza Fimbo.
Aidha,
Fimbo ameongeza kuwa TFDA imekuwa ikifanya tathmini na usajili wa
bidhaa kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama,
ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko.
"Kuwepo
kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji
wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.
Pia
tumeweza kusajili maeneo ya biashara za bidhaa za chakula, dawa,
vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kutambua maeneo ambayo
bidhaa hizo zinazalishwa, kuhifadhiwa, kusambazwa na kuuzwa. Mfumo huu
husaidia kuhakikisha kuwa maeneo husika yanakidhi vigezo ili kutoathiri
usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa". Alieleza Fimbo.
Aidha
ameongeza kuwa, TFDA katika kipindi cha miaka mitatu (2015/16 –
2017/18), imeweza kusajili jumla ya maeneo 25,630 ya biashara za bidhaa
zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na maeneo 9,000 yaliyosajiliwa mwaka
2016/17 na maeneo 5,606 mwaka 2015/16, hii ikiwa ni sawa na ongezeko la
60.5%.
Aidha, katika
kipindi hiki, TFDA imeendelea kushuhudia kufikiwa kwa dira yake ya kuwa
taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula,
dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi
mbalimbali kuja kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini
kwao.
(mfano nchi za
Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana,
Mauritius, Lesotho na Bangladesh zinekuja kujifunza TFDA).
"Katika
kipindi cha mwaka 2015/16 - 2017/18, Mamlaka imefanikiwa kufikia na
kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake.
Mamlaka
katika kipindi cha 2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika
utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika
Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili
kulinda afya ya jamii." Alieleza Fimbo.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kukamilika kwa jengo la Maabara na kufungwa kwa
vifaa vya kisasa vya uchunguzi jijini Mwanza jambo ambalo limesaidia
kusogeza huduma zaidi kwa jamii.
0 on: "TFDA YAJIVUNIA KUIPAISHA TANZANIA KWAKUWA NA MIFUMO BORA YA UDHIBITI"